1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Maafisa wa Black Water wapewa kinga

30 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BM

Wapelelezi wa wizara ya ulinzi ya Marekani wamependekeza mpango wa kinga kwa maafisa wa kampuni ya usalama ya Marekani Black Water inayohudumu nchini Irak.

Maafisa wa kampuni hiyo walihusika na mauaji ya raia 17 wa Irak ya tarehe 16 mwezi Septemba.

Hatua hiyo mpya itazuia juhudi za kuwafungulia mashtaka maafisa waliohusika.

Gazeti la Times la nchini Marekani limeripoti kwamba maafisa hao wameahidiwa kuwa hawatafunguliwa mashtaka ya aina yoyote kwa sharti kwamba watazungumza ukweli.

Mkuu wa kampuni hiyo Erik Prince amekanusha ripoti iliyotolewa na serikali ya Irak kwamba maafisa hao waliwafyatulia risasi raia wasiokuwa na hatia.