1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Mtuhumiwa wa ugaidi afutiwa mashtaka

5 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuf

Jaji wa mahakama nchini Marekani ametupilia mbali mashtaka dhidi ya mtuhumiwa wa ugaidi raia wa Kanada ambaye amefungwa katika jela ya Guantanamo Bay Cuba.

Serikali ya Marekani inamtuhumu Omar Khadr kwa kumuua kwa bomu la mkono afisa wa cheo cha sajini wa jeshi la Marekani, wakati wa msako wa wapiganaji wa kundi la Al Qaida nchini Afghanistan miaka mitano iliyopita.

Khadr ambaye wakati anakamatwa alikuwa na umri wa miaka 15, alikuwa akikabiliwa na mashtaka makubwa yakiwemo ya mauaji.

Lakini Jaji aliyatupilia mbali mashtaka hayo akisema kuwa Khadr hakuwa katika kundi la watu maharamia.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani pia imesema mashtaka ya ugaidi dhidi ya mfungwa mwengine katika jela ya Guantanamo Bay, ambaye alikuwa dreva na mlinzi wa Osma Bin Laden yamefutwa.