1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watalii wanne wa Ufaransa wauwawa.

25 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfzc

Nouakchot. Kusini mwa Mauritania watalii wanne kutoka Ufaransa wamepigwa risasi na kufa katika shambulio lililofanywa na watu wasiojulikana wenye silaha. Mtu wa tano katika kundi hilo amenusurika lakini amejeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa polisi katika mji wa Aleg, ambako tukio hilo lilitokea , watu hao wenye silaha waliwapora watalii wakitumia bunduki na baadaye waliwamiminia risasi. Watu waliofariki ni pamoja na watoto wawili. Mji wa Aleg uko kiasi cha kilometa 245 mashariki mwa mji mkuu wa Mauritania Nouakchot.