1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waumini wa kikristo kutoka kila pembe ya dunia wamemiminika Jerusalem ya mashariki kwa sherehe za Pasaka

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBI

Wawakilishi wa Israel na wale wa Hamas wamethiibitisha ripoti kuhusu maendeleo yaliyopatikana katika juhudi za kuachiliwa huru mwanajeshi wa kiisrael Gilad Schalit anaeshikiliwa mateka tangu miezi tisaa iliyopita.Msemaji wa Hamas FAWZI BARHUM amesema kuna dalili za kutia moyo katika mazungumzo ya kubadilishana wafungwa.Kupitia upatanishi wa Misri,Israel imekabidhiwa orodha ya majina ya wafungwa wa kipalastina wanaobidi kuachiliwa huru.Israel inasubiriwa kutoa jibu.Kwa mujibu wa duru za wapalastina,Hamas wanadai wapalastina zaidi ya elfu moja waachiwe huru.Muakilishi wa ngazi ya juu wa serikali ya Israel amethibitisha pia kupitia Radio Israel,”kuna ishara za maendeleo”,amesisitiza hata hivyo “bado kuna mengi ya kufanya kabla ya kuafikiana kubadilishana wafungwa.”

Mainz-Berlin:

Mwenyekiti wa baraza la maaskofu wa Ujerumani,Kardinal Karl Lehmann akihubiri wakati wa misa ya Pasaka ametoa mwito “wapatiwe fursa mpya hata wale waliofanya makosa yaliyofurutu.””Waliopotoka hawastahiki watu kuwakatia tamaa” amesema Kardinal Lehmann alipokua akihutubia misa katika kanisa kuu la Mainz. Mwenyekiti wa baraza kuu la kanisa la kiinjili Askofu Wolfgang Huber amesema kwa upande wake tunanukuu:”Sherehe za Pasaka ni dalili ya machipuko.Kutokana na imani zao za kidini,binaadam wanaweza ku kuepukana na hofu na hali ya akukata tamaa”-mwisho wa kumnukuu askofu Wolfgang Huber,aliyesema hayo katika misa ya pasaka katika kanisa kuu la mjini Berlin.

Maelfu ya waumini kutoka kila pembe ya dunia wamemiminika mashariki ya Jerusalem kusherehekea pasaka.Askofu mkuu Michel Sabbah aliongoza misa katika kanisa kuu la mji mkongwe wa Jerusalem.Katika risala yake ya Pasaka Askofu mkuu Michel Sabbah ametoa mwito umalizike ugonvi kati ya waisrael na wapalastina.Waumini wa madhehebu ya kigiriki ya Orthodox ,Armenia, na Koptik walisherehekea pia misa katika kanisa kongwe la Jerusalem-ambako wakristo wanaamini ndiko alikozikwa Jesus Kristo.Wakristo wachache tuu wa kipalastina ndio walioruhusiwa kushiriki katika sherehe hizo za Pasaka kutokana na vizuwizi vilivyowekwa na Israel.