1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Italia Romano Prodi ajiuzulu

25 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CxcC

Waziri mkuu wa Italia Romano Prodi amejiuzulu baada ya kushindwa katika kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.

Rais wa nchi hiyo, Giorgio Napolitano, amemtaka bwana Prodi aendelee na kazi yake huku akijiandaa kushauriana na viongozi wa kisiasa kuanzia leo mchana.

Romano Prodi mwenye umri wa miaka 68, licha ya kukabiliwa na pigo la chama cha kikatoliki cha UDEUR kujiondoa kutoka kwa serikali yake mapema wiki hii, aliamua kushiriki katika kura ya kutokuwa na imani naye, licha ya miito ya viongozi wa ngazi za juu, akiwemo rais Napolitano, kumtaka ajiuzulu.

Rais Napolitano kwa kushauriana na viongozi wa vyama na bunge, anaweza aidha kuitisha uchaguzi wa mapema au kuunda serikali ya mpito.

Waziri mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi, akipania kurudi madarakani baada ya miezi 20 ya kukaa katika upinzani, anataka uchaguzi wa mapema ufanyike.