1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan amejiuzulu

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUFn

Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan,Almazbek Atambayev amejiuzulu kabla ya uchaguzi wa bunge uliopangwa kufanywa Desemba 16.Kiongozi wa upinzani Atambayev,mwenye siasa za wastani aliongoza wimbi la maandamano dhidi ya Rais Kurmanbek Bakiyevin katika mwaka 2006,lakini mwezi Machi mwaka huu alikwenda upande wa pili na akajiunga na serikali.

Vyama 12,ikiwa ni pamoja na Social Democratic Party kinachomuunga mkono Atambayev vimejiandikisha kugombea uchaguzi wa mwezi ujao. Uchaguzi wa Desemba umeitishwa baada ya Kyrgyzstan kuanzisha katiba mpya katika mwezi wa Oktoba huku mivutano ya kisiasa ikiendelea katika nchi hiyo ya Asia ya Kati.