1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Uingereza akamilisha ziara nchini China

19 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cupe

BEIJING: Uingereza na China zitaanzisha enzi mpya ya ushirikiano kuhusu mazingira.Nchi hizo mbili zinatazamia kuongoza juhudi za kimataifa kwa azma ya kuhifadhi mustakabali wetu.Waziri Mkuu wa Uingereza,Gordon Brown alitamka hayo leo hii alipokamilisha ziara yake ya siku mbili nchini China.

Kinyume na siku ya Ijumaa aliposisitiza kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya madola hayo mawili,Brown leo alichunguza miradi ya miji ya Beijing na Shanghai.Kwa miradi hiyo,China inalenga kupunguza kwa sehemu kubwa gesi zinazotoka viwandani na kuchafua mazingira.