1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri nchini Urusi ajiuzulu-kisa ?

19 Septemba 2007

Kisa ni ujmaa na waziri mkuu.Waziri wa ulinzi wa russia ameamua kujiuzulu kwa kuwa waziri mkuu ni ba-mkwe wake.Amemuona binti yake.

https://p.dw.com/p/CH81

Waziri wa ulinzi wa Russia, Anatoli Serdjukov alijizulu hapo jana .Sababu ya kujiuzulu kwake, ni ujamaa wa karibu sana na waziri-mkuu Viktor Subko.Waziri wa ulinzi amemuoa mtoto wa kike wa waziri-mkuu na kwahivyo anaona hawezi kubakia waziri wa ulinzi.Kwa sasa,Serdjukov anabaki kwenye wadhifa wake hadi ijumaa ijayo ambapo baraza jipya la mawaziri litatangazwa mjini Moscow.

Sauti nyingi nchini Russia zinaona uamuzi alioukata waziri wa ulinzi Anatoli Serdjukov ni barabara kabisa na wa kidemokrasi.Rasmi ni kuwa kwavile waziri mkuu ni ba-mkwe wake, wanakuwa wanaleta ujaaa serikalini.Subkov asema:

„Kabla kuidhinishwa na Bunge kushika wadhifa wa waziri mkuu, nilizungumza na waziri wa ulinzi.Waziri wa ulinzi kama mjuavyo ni jamaa yangu mkubwa.Kwahivyo, tumeamua yeye amuarifu rais kwamba anahisi ni bora aachane na wadhifa wa waziri wa ulinzi.“

Alisema waziri mkuu mpya Viktor Subkov.

Rais Wladmir Putin wa Russia akaidhinisha uamuzi huo wa kujiuzulu kwa waziri wake wa ulinzi Serdjukov.Wanasiasa hapo wakashangiria.waziri wa ulinzi wa zamani Sergej Ivanov ,akasema binafsi anauheshimu uamuzi uliokatwa.

Swali linalochomoza hapa ni iwapo Serdjukov laiti haingekuwa waziri-mkuu ni bamkwe,angechaguliwa ijumaa ijayo kuwamo ndani ya Baraza jipya la mawaziri ?

Anafahamika kuwa ni mmangimeza na hapendezi. Hakuna matokeo yoyote ya kupendeza aliofanya tangu kushika madaraka hayo.

Lakini,mwanabiashara huyu wa zamani wa fanicha hana wasi wasi wala wahaka kwa maisha yake.Imefahamika karibuni hivi atashika wadhifa wa mwenyekiti katika Baraza la Usalama la taifa.

Katika wadhifa huo haioneshi ni kero kwa kuwa waziri mkuu ana ujamaa nae.

Hata mawaziri wengine hawana sababu ya kuingiwa na homa ya wasi wasi,kwani siku zao za baadae madarakani zitahakikishwa na rais Putin.Aliekua hadi sasa waziri mkuu ,Michail Fradkov ,anatarajiwa kupewa wadhifa mnono wa shirika la TRANSNEFT ambalo linamiliki mabomba ya mafuta ya petroli nchini.

Waziri wa viwanda na nishati Viktor Christenko,aweza kuchaguliwa mkuu wa kampuni kubwa la mafuta la ROSENEFT.

Dimitrij Medwedev ,makamo-waziri mkuu na anaegombea wadhifa wa urais baada ya Putin, aweza akashika wadhifa wa mkuu anaeugua wakati huu wa kampuni kubwa la Gesi (GAZPROM),Alexej Miller.

Shaka shaka bado ziko kwa waziri wa uchumi German Greff.Hata nae hatatupwa.

Baraza jipya la mawaziri la Russia,lazima litangazwe hadi ijumaa ijayo.Hadi hapo kuna wakati wa kutosha kuvumisha huyu atakuwa nani na nafasi gani ?