1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ulinzi wa Marekani afanya ziara ya ghafula Irak

5 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXYe

Waziri wa Ulinzi wa Marekani,Robert Gates amewasili Irak kwa ziara ambayo haikutangazwa hapo kabla.Katika majadiliano yake pamoja na Rais Jalal Talabani na waziri Mkuu Nuri al-Maliki, Waziri Gates atawahimiza viongozi hao kuharakisha mwenendo wa upatanisho wakati ambapo machafuko yanapunguka nchini humo.

Gates anataka kujua iwapo serikali ya Irak inayodhibitiwa na Washia itaweza kupatana na Wairaki wa madhehebu ya Kisunni ili sheria muhimu iweze kupitishwa kwa haraka,kuimarisha maelewano kati ya jamii hizo mbili.