1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WEISBADEN : Putin kuzuru Iran licha ya onyo la njama

16 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7FV

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema hapo jana ataitembelea Iran kujadili mpango wake wa nuklea licha ya kurepotiwa kuwepo kwa njama ya kutaka kumuuwa nchini humo.

Putin ameuambia mkutano wa waandishi wa habari baada ya mazungumzo yake na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani kwamba bila ya shaka anakwenda Iran na kwamba iwapo utachukuwa hatua kwa vitisho kadhaa na mapendekezo ya maafisa wa usalama hapo tena mtu itabidi abakie nyumbani tu.

Maafisa wa Ikulu ya Urusi hapo mapema walisema mipango ya ziara hiyo ya Putin iko mashakani baada ya shirika moja la habari la Urusi kuripoti kwa kukariri duru ya usalama bila ya kuitaja jina ikisema kwamba wala njama wanapanga kumuuwa Putin wakati akiwa Tehran.