1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WINDHOEK:Uvuvi wa sili waanza

6 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlI

Msimu wa kila mwaka wa kuvua sili nchini Namibia umeanza rasmi wiki hii huku wanaharakati wa kutetea haki za wanyama wakiupinga.Serikali kwa upande wake inalaumu wanaharakati hao kwa kutoa taarifa za kupotosha kwa makusudi.Kulingana na serikali kudhibiti idadi ya sili nchini humo ni muhimu kwa sekta ya uvuvi na nafasi za kazi zinazotoka na shughuli ya kuvua sili.

Nchi ya Namibia inasifika kwa wanyama wa pori na majangwa kando ya pwani ya bahari ya Atlantik ijulikanayo kama Skeleton Coast.Takriban sili laki nane u nusu wanaishi kwenye kundi la visiwa vilivyo eneo la pwani ya kusini mwa nchi.Msimu wa kuvua sili huanza Julai Mosi na kuchukua muda wa takriban miezi mitano.

Serikali ilitangaza wiki jana kuwa inaruhusu sili alfu 6 wa kiume waliokomaa kuuawa na kuongeza idadi ya watoto wa sili kwa alfu 20.Kwa mujibu wa serikali sili hao hula tani laki tisa za samaki kila mwaka kiwango ambacho ni zaidi ya thuluthi moja ya samaki wanaovuliwa na sekta ya uvuvi nchini humo.

Ripoti ya mwaka jana ya Benki Kuu ya Namibia inaonyesha kuwa sekta ya uvuvi ilichangia asilimia tano ya pato zima la kitaifa mwaka 2005.