1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wito kuweka kiwango kwa uwekezaji wa kigeni

4 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CX4q

Mkutano wa mwaka wa chama cha kihafidhina cha CDU cha Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel umemalizika hii leo mjini Hannover.Merkel amependekeza kuwa uwekezaji wa kigeni katika makampuni ya Kijerumani usipindukie asilimia 25, ikiwa uwekezaji huo utahatarisha maslahi ya taifa.Wajumbe wa CDU kwa wingi mkubwa,waliunga mkono pendekezo hilo.

Mkutano huo wa siku mbili ulifungwa kwa hotuba ya Erwin Huber,kiongozi mpya wa chama cha CSU ambacho ni chama ndugu cha CDU.Huber alisisitiza kuwa chama chake kinawajibika kushirikiana na CDU.Akaongezea kuwa vyama hivyo pamoja vitashinda uchaguzi wa mwaka 2009.