1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zoezi la kuhesabu kura , DRC laendelea

29 Novemba 2011

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo katika uchaguzi wa pili baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe,katika siku ya uchaguzi ambayo iligubikwa na hali ya mtafaruku na ghasia.

https://p.dw.com/p/13IjW
Watoto wakichungulia mkutano wa kampeni katika jamhuri ya kidemokrasi ya CongoPicha: AP

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo katika uchaguzi wa pili baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, katika siku ya uchaguzi ambao iligubikwa na hali ya mtafaruku, ghasia na madai ya udanganyifu. Watayarishaji wa uchaguzi huo wameendelea na uchaguzi huo wa rais na bunge katika nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati licha ya hofu kuwa uchelewesho wa kufikisha vifaa vya kupigia kura na malalamiko kuhusu hatua za uchaguzi huo utaleta hali ya malalamiko makubwa katika matokeo ya uchaguzi. Rais Joseph Kabila anakabiliwa na upinzani wa wagombea kumi, ukiongozwa na mwanasiasa wa siku nyingi wa upinzani Etienne Tshisekedi. Kiasi ya watu 18,000 wanagombea uchaguzi huo kuwania viti 500 katika bunge la Congo. Baadhi ya karatasi za kupigia kura ni jumla ya karatasi kadha kwa hiyo maafisa walipaswa kupitia kila karatasi ili kuangalia alama ya x ya mpiga kura.

Matokeo ya mwanzo yanatarajiwa kutolewa Desemba 6.