Deutsche Welle: Timu ya taifa ya soka ya Mali kupambana na Ghana kesho kuwania nafasi ya tatu ya mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika ya kandanda.
Kutana na wanawake hawa wenye ulemavu waliamua kujiingiza kwenye mchezo wa mpira wa mikono na namna wanavyosakata mchezo huo.
Ligi Kuu ya Kandanda hapa Ujerumani - Bundesliga inaelekea ukingoni. Baada ya bingwa kujulikana sasa macho yote yamegeuka katika nafasi za kucheza kandanda la Ulaya. Kwa mengi zaidi kuhusu mechi za wikiendi hii Suleman Mwiru amezungumza na Bruce Amani kuhusu michezo ya wikiendi hii na ambao utatangazwa mubashara kupitia ukurasa wa Facebook wa DW Kiswahili na kupitia redio mbalimbali washirika.
Watu wasiopungua 7 wamekufa leo na wengine 21 wamejeruhiwa baada ya gari la mashindano kuparamia kundi la watazamaji waliofurika kwenye uwanja wa michezo mjini Colombo nchini Sri Lanka.