1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

15 wauawa katika shambulio la kigaidi Iraq

22 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CvwC

BAIJI:

Kwa uchache watu 15 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya mtu aliejitolea mhanga kujilipua wakati wa mazishi karibu na mji wa kaskazini mwa Iraq wa Baiji.Polisi imesema kuwa mshambuliaji aliingia katika hema iliokuwa imejaa na waombolezaji waliokusanyika kwa ajili ya mazishi ya afisa wa mkoa huo, kabla ya kujilipua.Hakujatokea kundi lolote kudai kuhusika na shambulio hilo.Lakini polisi imesema kuwa shambulio hilo linafana kufanywa na kundi la kigaidi la al-Qaida nchini Iraq.