Deutsche-Welle:Katika kombe la mataifa barani Afrika,vumbi litatimuliwa leo hii na Libya itakayoteremka uwanjani dhidi ya Senegal na Guinea ya Ikweta dhidi ya Zambia
Wenyeji Ivory Coast watalazimika kusubiri nusra kwa kutegemea matokeo mengine ili kuepuka kuondolewa katika hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON.
Ghana imefanikiwa kulazimisha sare ya mbili kwa mbili na kinara wa soka ya Afrika, Misri, katika mechi ya usiku wa Alkhamis, baada ya Mohammed Kudus kuyaweka kimiani magoli yote mawili ya Nyota hao Weusi.
Jumuiya ya uchumi ya Afrika ya Kati imesitisha uanachama wa Gabon kwa sababu ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika Agositi 30 ambapo rais Ali Bongo aliondolewa madarakani.