1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA:Rais Yar'Adua ateuwa baraza lake la mawaziri

27 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeo

Rais Umaru Yar’Adua wa Nigeria ameliteuwa baraza lake jipya la mawaziri 39.

Yar’Dua amewaonya mawaziri wake kuwa hata vivumilia vitendo vya rushwa katika serikali yake.

Rais wa Nigeria amewateuwa pia mawaziri wadogo watatu watakaohudumu chini yake katika kusimamia mapato yanayotokana na mafuta, Gesi na Umeme.

Baraza hilo la mawaziri 39 lina mchanganyiko wa mawaziri wenye taaluma mbali mbali.

Shirika la kimataifa la kupambana na rushwa Transparency International katika ripoti yake ya mwaka 2006 lili ipa Nigeria alma 2.2 pekee kati ya jumla ya alama 10 katika jitihada za kupambana na rushwa nchini humo.