1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATHENS : Putin kusaini mkataba wa bomba la mafuta

15 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIr

Rais Vladimir Putin wa Urusi anaitembelea Ugiriki ambapo anatazamiwa kusaini mkataba na Ugiriki na Bulgaria kujenga boma la kupitishia mafuta ya Urusi kutoka Bahari Nyeusi kwenda bahari ya Aegean.

Kazi ya ujenzi wa bomba hilo lenye urefu wa kilomita 280 inatazamiwa kuanza mwakani baada ya miaka 15 ya majadiliano yaliokuwa yakisuasua.

Mataifa hayo matatu yamelazimika kuanza ujenzi huo kutokana na kupanda mno kwa bei za mafuta na mradi mwengine wa bomba la mafuta la Baku-Ceyhan kwenda bahari ya Mediterrranean ambalo linapitia Urusi.