1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azimio la UM juu ya Dafur

1 Agosti 2007

Mwishoe Baraza la Usalama la UM limepitisha azimio kutuma Dafur,Sudan askari 26,000 wa kuhifadhi amani .Iwapo watamudu kumaliza mauaji ni swali jengine-asema Stefanie Duckstein:

https://p.dw.com/p/CHAC

Mauaji mkoani Dafur,magharibi mwa Sudan yameshachukua maisha ya watu laki 2 hadi sasa.Zaidi ya wakaazi milioni 2 wa Dafur wametimuliwa maskani mwao na wamekimbiza roho zao.

Kusitasita,kuzingatia mambo na kubishana kumesababisha hasara kubwa ya maisha.Ilihitaji majaribio mengi kupita kiasi katika Baraza la Usalama la UM ili kuweza mwishoe, hivi sasa kupitisha azimio ambalo Katibu mkuu wa UM Ban Ki Moon ameliita la “kihistoria”.

Imeafikiwa sasa kutuma Dafur kikosi cha askari 26,000 wa kuhifadhi amani na kukomesha mauaji ya halaiki ya watu huko Dafur.Hili ni jukumu ambalo hadi sasa vikosi viliopo huko vya UA visivyo na zana wala fedha za kutosha vilishindwa kumudu.

Lakini lile azimio ambalo, chombo cha hadhi ya juu kabisa ya doplomasia ya kimataifa kimekieleza ni kitendo cha “historia”, ni hatua hafifu kwani imetokana na muafaka wa pande zote zilizohusika.Ni muafaka wa wanachama 15 wa baraza la Usalama.

Ilikua Uingereza na Ufaransa zilizufungua mlango kutungwa mswada wa azimio hilo usio mkali ambao haukutaja hujuma zinazoselelea za vikosi vya serikali ya Sudan wala zile za wanamgambo wa Janjaweed.

Ni maridhiano kwavile, vikosi vinavyosimamia amani havina mamlaka ya kumpokonya yeyote silaha zisizo halali.

Marufuku ya kuuziwa silaha Sudan iliowekewa, ni dhaifu na hayataheshimiwa na dola kama China au Russia.

Kulazimisha azimio kali zaidi kungetiwa munda na kura ya veto ya China au Russia.Kwani, serikali ya China inaona azimio kali la aina hiyo si muwafaka wakati huu na China kwa kuzuwia kura yake ikilikwamisha mara kwa mara.

Ushahidi uliotolewa mara kwa mara na vyama vya haki za binadamu ili kuthibitisha kuhilikishwa watu nchini Sudan na kuitwika serikali ya Sudan jukumu la hayo, hakujaleta matokeo yoyote.

Chini ya hali hii, azimio la UM lililopitishwa jana kwa sasa iangaliwe ni ishara tu iliotoa diplomasia ya magharibi.Hakuna maana ndio mwisho wa kuhilikishwa umma huko Dafur.Mabingwa wanadhani, utapita mwaka hadi kikosi hicho kikubwa kabisa hadi sasa cha UM kuanza kazi.Mwaka,ambamo mengi yaweza kutokea.