1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Shambulio la bomu Irak limeua wanane

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCl1

Nchini Irak,bomu lililotegwa ndani ya gari, limeripuka Kerbala,mji mmojawapo ulio takatifu kwa Washia.Si chini ya watu 8 wamefariki na 30 wengine wamejeruhiwa.Polisi inasema,mripuko huo ulitokea nje ya jengo takatifu la Al-Abbas.Mji wa Kerbala upo kama kilomita 80 kusini ya mji mkuu Baghdad.