BAGHDAD: Shambulizi la gesi ya klorini limeua 3
17 Machi 2007Matangazo
Nchini Irak watu wasiopungua 6 wameuawa katika shambulio lililotumia gesi ya klorini. Askaripolisi 2 ni miongoni mwa hao waliofariki. Inasemekana kuwa kama watu 350 wamejeruhiwa vile vile.Kwa mujibu wa ripoti ya majeshi ya Marekani,washambulizi 3 waliyojitolea muhanga walijiripua katika magari ya kusafirishia gesi ya klorini.