1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Wimbi la ghasia kaskazini mwa Iraq

26 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMb

Wimbi jipya la ghasia limeyakumba maeneo ya kaskazini mwa Iraq ambapo watu 15 wameuwawa kwa mujibu wa ripoti za leo.

Katika kijiji kilichoko karibu na Qadaa Sinjar kwenye mkoa wa Nineveh kiasi kilomita 250 kutoka mji mkuu Baghdad raia 10 waliuwawa na wengine tisa wamejeruhiwa kwenye shambulio la bomu la kutegwa ndani ya gari.

Eneo la Qadaa Sinjar linakaliwa na watu wengi wa jamii ya Yazidi ambayo haifuati maadili ya dini ya Kislamu.Vijiji vinavyokaliwa na jamii hiyo vilikuwa vikishambuliwa mara kwa mara katika mwezi wa Agosti ambapo kiasi cha watu 500 waliuwawa kwenye mfululizo wa mashambulio ya mabomu.