1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING : China yashutumiwa kwa jaribio la kombora

20 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZX

China inakabiliwa na shutuma za kimataifa kutokana na jaribio la kombora lililorepotiwa kufanyika katika anga za juu wiki iliopita.

Japani imeelezea wasi wasi wake kadhalika Marekani na Australia.Inadhaniwa kwamba China ilitumia kombora la masafa ya kati kutoka ardhini kuteketeza satalaiti ya uchunguzi wa hali ya hewa kwenye anga za juu ambayo ilirushwa hapo mwaka 1999.Wachambuzi wa mambo wanasema hili ni jaribio la kwanza la kombora la kudungulia satalaiti kuwahi kufanyika katika kipindi cha miaka 20.

Wizara ya mambo ya nje ya China imekataa kuthibitisha au kukanusha repoti hizo.

Iwapo itathibitika kufanyika kwa jaribio hilo itamaanisha kwamba China hivi sasa kinadharia inaweza kuzindunguwa satalaiti zozote zile zinazoendeshwa na mataifa mengine.