1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Hezebollah na mzozo mpya wa kisiasa nchini Lebanon

20 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCr8

Kiongozi wa kundi la Hezebollah nchini Lebanon, Hassan Nasrallah, amesema kuna njia mbili za kuusuluhisha mzozo wa kisiasa nchini Lebanon. Akiuhotubia mkutano wa hadhara wa wafuasi wake katika mji mkuu Beirut, Nasrallah amesema aidha ni kuunda serikali ya umoja wa taifa au kuitisha uchaguzi wa mapema. Serikali ya Lebanon imeingia katika msukosuko wa kisiasa kufuatia kujiuzulu mawaziri 6 wa chama hicho cha Hezebollah kinachoungwa mkono na Syria.

Viongozi wa Hezebollah wamesema serikali ya Lebanon ni serikali sioweza kutetewa na wametishia kuitisha maandamano makubwa ya raia.