1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BELGRADE:Spika wa bunge la Serbia aachia ngazi

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2I

Spika mwenye msimamo mkali wa bunge la Serbia Tomislav Nikolic amejiuzulu baada ya kushikilia nafasi hiyo kwa muda wa siku tano pekee.

Kuondoka kwa bwana Tomislav wa chama cha Kizalendo ni sharti la makubaliano yaliyofikiwa ijumaa iliyopita kati ya vyama viwili vikuu vinavyotarajia kuunda serikali ya mseto.

Hatua hii inatoa nafasi kwa bunge la nchi hiyo kupiga kura juu ya baraza la mawaziri la serikali mpya ya mseto ambalo litaidhinishwa jumanne.

Vyama vinavyounda mseto huo lazima viunde serikali ifikiapo tarehe 15 mwezi huu ikiwa ni kiasi miezi miine baada ya uchaguzi wa bunge.

Mataifa ya magharibi yamekuwa yakizungumzia wasiwasi wake juu ya kuchaguliwa bwana Nicolac kuwa spika na kuhofia kwamba nchi hiyo huenda ikaachana na mchakato wa mageuzi.

Wadhifa wa Spika nchini Serbia unashikilia nafasi ya tatu ya nyadhifa zenye usemi mkubwa kwenye masuala ya uongozi.