1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Urusi yazidi kulaumiwa kwa kufunga bomba lake la mafuta

10 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCc6

BERLIN

Umoja wa Ulaya na Ujerumani ambayo kwasasa ndiyo mwenyekiti wa umoja huo, zimeulaumu uamuzi wa Urusi kusitisha kupeleka mafuta katika nchi nyingine za Ulaya kupitia Belorussia.

Kansela wa Ujerumani Angela Markel amesema kuwa uamuzi huo wa haukubaliki, kwani Urusi ilitakiwa kwanza kushauriana na nchi husika.

Hapo siku ya Jumatatu Urusi ilitangaza kusitisha usafirishaji wa mafuta kwa bomba linalopitia Belorussia, ikidai kuwa nchi hiyo inafyonza mafuta hayo, kinyume cha sheria.Belorussia kwa upande wake inataka Urusi ilipe dola 45 kwa kila tani ya mafuta kama kodi kwa bomba hilo kupita katika ardhi yake, kitu ambacho Urusi haikubalini nacho.

o.