1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA:AU yalitaka kundi la FNL kurudi kwenye mazungumzo ya amani

30 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUc

Umoja wa Afrika umelitaka kundi la mwisho la uasi nchini Burundi linalopingana na serikali la FNL Palipehutu kujiunga tena na kundi linalojadili makubaliano ya amani na kusaidia kuuokoa mpango huo kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Kundi la FNL lilijiondoa kwenye mazungumzo hayo mwezi uliopita na kutoweka hali ambayo iliibua wasiwasi kwamba huenda wamerejea msituni kwa lengo la kutaka kuanzisha tena mapigano.

Kwa mujibu wa Charles Nqakula mpatanishi kutoka Afrika kusini katika mazungumzo hayo ya Burundi,Umoja wa Afrika unataka shughuli hiyo imalizike kufikia desemba 31.Hapo jana rais wa Burundi Pirre Nkurunzinza alilitaka kundi hilo kurudi kwenye mazungumzo akisema serikali yake iko tayari kuheshimu muda uliowekwa wa kumalizika mazungumzo.