1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA:Mapigano katika kundi la FNL

4 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSk

Kumetokea mapigano mapema leo nchini Burundi kati makundi yanayopinga ndani ya kundi la waasi la FNL ambapo askari waasi sita wameuawa:

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters mapigano hayo yalitokea kwenye maeneo ya Buterere nje kidogo kaskazini mwa mji mkuu wa Bujumbura.

Inaarifiwa kuwa waliyouawa ni wapiganaji wanaompinga kiongozi wa kundi hilo la Forces for National Liberation FNL Agathon Rwasa.