1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Senate laidhinisha mswada wa dola bilioni 700

2 Oktoba 2008

Bunge la Senate nchini Marekani limeidhinisha mswada wa dola bilioni mia 7 unaolenga kuokoa soko la fedha linalokabiliwa na matatizo.

https://p.dw.com/p/FSXt
Seneta Harry Reid kiongozi wa chama cha Demokratik kwenye Bunge la SenatePicha: AP

Bunge hilo liliidhinisha mswada kwa kura 74 kwa 25.Kiongozi wa Chama cha Democratik kwenye Bunge la Senate Harry Reid amesisitiza kuwa mswada huo umeimarishwa na si wa chama

Cha Republikan wala Democratik bali raia wote wa Marekani.Amesisitiza kuwa mswada huo una azma ya kuwapunguzia kodi raia wa Marekani.

Chini ya mpango huo mpya wa kuokoa jahazi la uchumi wa Marekani serikali itaweza kununua taasisi zinazokabiliwa na matatizo ya fedha.Mswada huo kwa sasa unasubiri kuidhinishwa rasmi na Baraza la Wawakilishi hapo kesho.

Mwanzoni mwa wiki hii mswada huo ulipingwa vikali na wabunge wa upande wa Republikan jambo lililosababisha msukosuko wa bei katika masoko ya hisa ulimwenguni.Mzozo huo wa fedha umesababisha benki kubwa kabisa ya Marekani ya Lehmann Brothers kutangaza muflis nayo Benki ya Washington Mutual kuuziwa Benki ya JPMorgan Chase.