1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COTABATO: Watu sita wauwawa katika shambulio la bomu

11 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3y

Maofisa wa serikali nchini Ufilipino wamesema bomu la tatu limeripuka kusini mwa nchi hiyo mapema leo. Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika kisa hicho.

Hapo jana waatu wanaotuhumiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Al Qaeda walifanya shambulio la bomu lililowaua watu sita kwenye sherehe.

Bomu la nne lililogunduliwa katika eneo hilo limetenguliwa. Kufikia sasa hakuna kundi lolote lilitangaza kuhusika na mashambulio hayo.