1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM:Benki ya Dunia yatoa dola milioni 60 kupambana na malaria

6 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlP

Benki ya Dunia imeidhinisha msaada wa dola milioni 60 ili kusaidia nchi ya Tanzania kupambana na malaria vilevile kugharamia mafunzo ya wafanyikazi wa huduma za afya katika maeneo ya vijijini.

Kulingana na benki hiyo dola milioni 25 zitatumika kununulia vyandarua vya mbu vilivyotiwa dawa kupunguza ueneaji wa malaria.Dola milioni 35 zilizosalia zitatumika kutoa mafunzo kwa wafanyikazi wa huduma za afya katika mabaraza 121 ya wilaya.

Nchi ya Tanzania ina wakazi milioni 40.