1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Maafisa wawili wa polisi wauwawa kwenye shambulio la bomu

2 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNG

Maofisa wawili wa polisi wameuwawa kwenye shambulio la bomu mjini Multan nchini Pakistan. Watu wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye mripuko uliosababishwa na bomu hilo lilikuwa limetegwa kando ya barabara.

Mmoja wa majeruhi ni jaji ambaye hushughulikia sana kesi kuhusu ugaidi. Duru za polisi zinasema mabomu yaliyofungwa kwenye baiskeli yaliilenga motokaa ya jaji huyo.

Shambulio hilo limefanyika wiki mbili baada ya mtu wa kujitoa mhanga maisha kujiripua ndani ya mahakama katika mji wa Quetta, kusini magharibi wa Pakistan. Jaji mmoja na watu wengine 15 waliuwawa kwenye hujuma hiyo.