1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jaribio jengine la kombora lenye nguvu za kinuklea la Pakistan

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsG

Islamabad:

Pakistan imefanya jaribio jengine la kombora la masafa ya wastani siku moja tuu baada ya duru mpya ya mazungumzo ya amani pamoja na India.Msemaji wa kijeshi amesema mjini Islamabad jaribio hilo limefanikiwa..India na nchi nyengine jirani ziliarifiwa kabla ya hapo,msemaji huyo ameshadidia.Kombora hilo chapa Hatf nambari 5 lina uwezo wa kupiga hadi umbali wa kilomita 1300.India na pakistan zimekua kila kwa mara zikifanya maajaribio ya makombora yao.