1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel lafanya hujuma nyingine katika eneo la Gaza

21 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CehS

GAZA:

Jeshi la Israel limesema kuwa vikosi vyake vimewauwa wapiganaji wa Kipalestina 7 katika eneo la Gaza.Israel inasema imefanya hivyo kwa ajili ya kuzuia uvurumishwaji wa maroketi hadi Israel.Siku ya alhamisi maroketi matatu yalivurumishwa katika mji wa mpaka wa Israel.Mapema wiki hii,hujuma kadhaa za ndege za Israel,zimewauwa wapiganaji 12 katika eneo la Gaza,mkiwemo makamanda wawili wandamizi wa kundi la Islamic Jihad.