1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: 17 wauwawa kwenye shambulio la kujitoa muhanga

11 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBk3

Serikali ya Afghanstan imefahamisha kuwa mshambuliaji wa kujitoa muhanga ameua watu 17 akijaribu kuwalenga wanajeshi wa Uholanzi wa kikosi cha NATO waliokuwa wakishika doria kwenye soko moja lililoko kusini mwa jimbo la Uruzgan.

Waasi wakitaliban wamedai kuhusika na shambulio hilo lililotokea kwenye mji wa Deh Rawud.Watu 35 walijeruhiwa wakiwemo wanajeshi saba wa Uholanzi.

Duru zinasema wengi waliouwawa walikuwa watoto wa shule.

Umoja wa mataifa na maafisa wa jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO wamelaani shambulio hilo.