1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. NATO yachukua jukumu la uongozi wa jeshi la kulinda amani.

5 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5v

Shirika la kujihami la mataifa ya magharibi NATO linachukua jukumu la kuongoza vikosi vyote vya jeshi la kimataifa la kulinda amani nchini Afghanistan ISAF leo, wakati wanajeshi wapatao 12,000 wanaoongozwa na Marekani katika eneo la mashariki ya nchi hiyo wanakabidhiwa rasmi kwa uongozi huo wa NATO.

Hatua hiyo itaongeza idadi ya wanajeshi wa jeshi hilo la ISAF hadi kufikia wanajeshi 33,000 na kukamilisha kusambaa kwake nchini humo katika hatua ambayo jeshi la NATO inaieleza kuwa ni muhimu katika historia yake.

NATO hata hivyo inapata taabu kupata wanajeshi wa ziada ili kuweza kupambana na hali inayozidi kuongezeka ya mashambulizi ya taliban kusini mwa Afghanistan na kuimarisha ujenzi mpya wa nchi hiyo.

Wanajeshi 8,000 wengine wa Marekani ambao bado wako katika eneo la mashariki, watabakia chini ya uongozi wa jeshi linaloongozwa na Marekani ambalo litatumika katika shughuli za kupambana na ugaidi. Ujerumani inawajeshi karibu 2,800 ambao wako kaskazini mwa Afghanistan.