1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Wapiganaji wakataa pendekezo la rais.

1 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBLF

Wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan wamekataa pendekezo la rais Hamid Karzai la mazungumzo ya amani.

Msemaji wa Taliban amesema kuwa hakutakuwa na majadiliano wakati majeshi ya kigeni bado yako nchini humo. Rais Hamid Karzai amesema kuwa yuko tayari kukutana na viongozi wa waasi binafsi na kuwapa nafasi katika serikali iwapo wataacha mapigano. Hata hivyo , amesema pia kuwa suala la kuyaondoa majeshi yaliyowekwa na Marekani na majeshi ya kujihami ya mataifa ya magharibi NATO halina nafasi.

Wakati huo huo , mapigano na mashambulizi ya anga nchini Afghanistan yameuwa kiasi cha wapiganaji 14 wa Taliban .