1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Wanavijiji 30 wameuawa jimbo la mgogoro Darfur

14 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCt4

Vikosi vya Umoja wa Afrika vinavyolinda amani katika jimbo la mgogoro la Darfur,magharibi mwa Sudan vimesema hadi watu 30 wameuawa na wengine 40 wamejeruhiwa katika mashambulio yaliofanywa na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali.Watu wenye silaha waliopanda farasi na ngámia walikishambulia kijiji cha Sirba karibu na mpaka wa Chad na waliua kila alieonekana.Wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na serikali ya Khartoum wamelaumiwa kuhusika na mashambulio hayo.Umoja wa Afrika una kikosi cha amani cha wanajeshi 7,000 katika Darfur lakini kimeshindwa kukomesha mashambulio.Umoja wa Mataifa umesema utatoa Dola milioni 77 kuusaidia Umoja wa Afrika kugharimia vikosi zaidi na zana.Sudan imepinga mpango wa Umoja wa Mataifa uliopendekeza kupokea ujumbe wa kulinda amani huko Darfur.