1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinyanganyiro cha kombe la kilabu bingwa ya dunia

Mohammed Abdul-Rahman5 Desemba 2007

AC Milan ya Italia yataka kulipiza kisasi mbele ya Boca Juniors ya Argentina.

https://p.dw.com/p/CXTO

Historia ndiyo inayoiandama AC Milan wakati ikiwania alau safari hii kuibuka na matokeo ya kufurahisha na kumaliza janga la kushindwa timu za ulaya katika mashindano ya kombe la dunia la vilabu nchini Japan yanayozikusanya kilabu bingwa za mabara tafauti. Milan ingali ikikumbuka kipigo ilichokipata mbele ya Boca Juniors ya Argentina 2003.

Mara nyingi ni timu ya Amerika kusini zinazotamba katika mashindano hayo ya kilabu bingwa ya dunia. Itakumbukwa Barcelona ya Uhispania na Liverpool ya Uingereza ama England zilitolewa na wapinzani wao kutoka Brazil, licha ya kutawala fainali mbili za mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la kandanda la kimataifa –FIFA.

Mabingwa wa Amerika kusini Boca Juniors ya Argentina wanajiunga na Milan katika hatua ya nusu fainali wakijipa matumaini baada ya kulikosa taji la ubingwa nyumbani hivi karibuni.

Mshambuliaji kutoka Brazil Kaka ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa kuvutia duniani wakati huu na anayelisakata gozi katika kilabu ya AC Milan ya Italia anasema hakusahau bado kushindwa na Boca Juniors. Akaongeza kwamba barani ulaya kipa umbele na kunyakua ubingwa wa Champions League , lakini sasa Milan inataka kuwa kilabu bingwa ya dunia mashindano.

Kaka akasema wanataka kulipa kisasi safari hii baada ya kulazwa na Boca mwaka miaka minne iliopita kwa mikwaju ya Penalty.

Boca haitacheza nusu fainali dhidi ya Etoile Sahel au Pachuca ya Mexico hadi tarehe 12, wakati Milan itaingia uwanjani baadae.

Waitakare United ya New Zeland itaumana na Sepahan mabingwa wa Iran Ijumaa katika mchezo wa kufungua dimba chini ya mpango mpya wa timu saba na msindi kuumana na urawa Reds kutoka Japan katika robo fainali

Urawa waliilaza Sepahan mwezi uliopita katika fainali ya ligi ya mabingwa wa Asia . Kocha wa kilabu hiyo ya Iran Luka Bonacic alisema watafurahi kukutana nao tena .

Mabingwa wa Afrika Etoile du Sahel ya Tunisia na Pachuca ya Mexico wanaumana katika robo fainali Jumatatu ijayo, mechi ambayo huenda isipate shauku kubwa ya mashabiki wa kandanda wa Japan.

Kiwango cha soka wakati wa fainali mbili zilizopita za mashindano hayo ya kombe la kilabu bingwa ya dunia kilikua cha chini na kusababisha sehemu kubwa ya viwanja kuwa vitupu. Hata rais wa FIFA, Sepp Blatter alikiri mwaka jana kwamba kiwango cha Auckland City kilabu ya wachezaji wa ridhaa ya New Zeland hakikusaidia kuyapa shauku katika mashindano hayo.

Pamoja na hayo fainali mb ili zilizopita zilikua za kusisimua wakati International ilipoibwaga Barcelona 1-0 mwaka jana na Sao Paulo kuondoka na ushindi sawa na huo mbele ya Liverpool mwaka uliotangulia 2005.

FIFA iliandaa fainali za mashindano hayo ya dunia ya vilabu bingwa 2000 wakati Corithians ya Brazil ilipolinyakua kombe hilo, lakini kasi ikafifia katika mashindano hayo baada ya FIFA kukosa mshirika wa kibiashara.

Wakati wa mashindano hayo ya Japan , FIFA itafanya majaribio ya mpira mdogo kwa utaalamu mpya wa kiufundi kuona kama ufundi utasaidia kuondoa mabishano iwapo mpira ulivuka chaki langoni au la , ili ufundi huo uweze kutumiwa katika fainali za kombe la kandanda la dunia 2010 nchini Afrika kusini,

Wakati huo huo nje imefahamika kwamba mabingwa wa Afrika Etioile sahel wataumana katika mchezo wa kwanza kulitetea taji lao, ama na kilabu ya CF Ouagadougou ya Burkina faso au mabingwa wa Senegal AS Dounes. Mchezo wa kwanza utakua mjini Tunis mwishoni mwa juma kati ya machi 21 na 23 .

Makamu bingwa wa Afrika Al Ahli ya Misri watatoana jasho ama na timu ya Eritrea au ile ya Kenya. Al Ahli ilipoteza nafasi ya kuwa kilabu ya kwanza kushinda kombe hilo la kilabu bingwa Afrika kwa miaka mitatu mfululizo, ilipokandikwa na Etioile Sahel mwezi uliopita mjini Cairo na kilabu hiyo ya Tunisia kuondoka na kombe hilo.