1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIRKUK: Watu 80 wameuwawa katika shambulio la bomu

16 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBi0

Takriban watu 80 wameuwawa katika shambulio la bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji wa kaskazini wa Kirkuk nchini Irak.

Watu wengine 100 wamejeruhiwa katika shambulio hilo la kujitoa muhanga.

Mashambulio mawili yalilenga ofisi ya chama cha kisiasa cha Patriotic Union of Kurdistan kinacho ongozwa na rais wa Irak Jalal Talabani, na soko la nje lililo karibu na ofisi za chama hicho.

Polisi wamesema huenda idadi ya watu waliojeruhiwa ikaongezeka.

Wakati huo huo watu wengine tisa wameuwawa katika mfululizo wa mashambulio katika mji mkuu wa Baghdad. Mashambulio hayo yametokea huku wanajeshi wa Marekani wakiwa wameanzisha operesheni mpya kusini mwa Baghdad inayowahusisha askari 8,000 yenye lengo la kuzuia uingizaji wa silaha na wapiganaji wenye msimamo mkali katika eneo hilo la kusini.