1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya kombe la mataifa ya Ulaya 2008

2 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVmK

Lucerne:

Fainali za kombe la mataifa ya Ulaya 2008:

Kura ya michuano ya makundi katika fainali za kombe la mataifa ya ulaya 2008 imepigwa adhuhuri ya leo mjini Lucerne-Uswisi. Kwa mujibu wa kura hiyo ya mashindano yatakayoandaliwa kwa ubia kati ya Uswisi na Austria. Ujerumani imepata afueni kwa kupangwa katika kundi B zikiwemo pia Poland, Croatia na mwenyeji Austria.

Mwenyeji mshirika Uswisi imo katika kundi A pamoja na Jamhuri ya Cheki, Ureno na Uturuki. Kundi gumu ni lile linalozijumuisha Uholanzi, Ufaransa na mabingwa wa dunia Italia.

Fainali hizo za kombe la mataifa ya ulaya 2008 zitaanza Juni 7 hadi 29 katika miji ya Basel, Berne Zurich na Geneva kwa upande wa Uswisi na nchini Austria ni Innsbruck, Klagenfurt, Salzburg na Vienna uwanja utakaochezwa mechi ya mwisho ya fainali. Mabingwa watetezi ni Ugiriki watakaoumana na Sweden , Uhispania na Urusi katika kundi D.