1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Watu waandamana nchini Uingereza kupinga gereza la Marekani la Guantanamo.

11 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbe

Maandamano yamefanywa nje ya ubalozi wa Marekani mjini London, Uingereza kupinga gereza la Marekani la Guantanamo liloloko Cuba.

Maandamano hayo yamefanywa miaka mitano tangu gereza hilo, ambalo lina wafungwa takriban mia nne washukiwa wa ugaidi, lilipoanzishwa.

Mvulana wa umri wa miaka kumi, Anas Al-Banna, ambaye baba yake anashikiliwa katika gereza la Guantanamo, amewasilisha barua kwa afisi ya Waziri Mkuu, Tony Blair, akimtaka asaidie kuhakikisha babake ameachiliwa.

Jamil al-Banna, mwenye umri wa miaka arobaini na minne, amekuwa akishikiliwa katika gereza la Guantanamo tangu miaka minne iliyopita.

Marekani inawachukulia baadhi ya wafungwa hao kuwa maadui wa kivita na hivyo kuwanyima haki nyingi za kimsingi, kulingana na sheria za kimataifa.

Hatua hiyo ya Marekani imesababisha upinzani mkali mara kwa mara kutoka kwa makundi ya kuetetea haki za binadamu.

Maandamano yalikuwa yamepangwa kufanywa katika maeneo kadhaa duniani kupinga gereza hilo la Guantanamo.