1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yaripotiwa karibu na makazi ya Gaddafi

22 Agosti 2011

Mapigano makali yameripotiwa kutokea karibu na nyumbani kwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi mjini Tripoli, ikiwa imepita siku moja baada ya vikosi vya waasi kushangilia kufanikiwa kuingia katikati ya mji huo.

https://p.dw.com/p/12LAn
Moshi umetanda mjini TripoliPicha: dapd

Kwa nyakati tofauti, mapigano hayo pia yamesikika kusini mwa Tripoli, ambapo kumekuwa na majibishano ya silaha nzito na risasi. Awali viongozi wa waasi walitahadharisha uwepo wa vikwazo kutoka kwa wanajeshi wa Gaddafi ingawa kwa kiasi kikubwa wamemalizwa.

Bürgerkrieg in Libyen Erfolg der Rebellen HOCHFORMAT + ARCHIV
Mtoto wa Gaddafi, Seif al-IslamPicha: dapd

Hakika mpaka sasa bado haijajulikana alipo kiongozi huyo wa Libya, ingawa mmoja kati ya watoto wake, Seif al-Islam amekamatwa na mwengine Mohamed Gaddafi alisika akiihojiwa na televisheni ya Al-Jazeera akiwa amejikunyata nyumbani kwake akihogopa kuondoka.

Katika mahojiano hayo Mohamed alikiri kwamba utawala wa baba yake umefanya makosa huku akisema yeye hakuwa katika sehemu ya maafisa wa usalama, wa nafasi yeyote itakoyaomwezesha kujua kinachoendelea.

Hapo jana Gaddafi alisikika akitoa kauli za kukaidi kuondoa nchini humo kwa mara tatu tofauti. akzingumza kwa jazba alisikia akisema hatosalimu amri, na kuwataka watu wa Tripoli kuwa madhubuti kuulinda mji huo.

Lakini kiongozi huyo hajaonekana hadharaini kwa wiki kadhaa sasa. Chanzo kimoja cha Kidiplomasia kinasema kiongozi huyo anaweza kuwepo katika makazi yake yaliyopo katikati ya Bab al-Aziziya katikati ya mji wa Tripoli.

Kwa upande wao Umoja wa Kujihami wa NATO ambao unaoongoza operesheni ya anga nchini Libya, umesema pamoja na mambo mengine operesheni ya anga itaendelea mpaka majeshi ya Gaddafi yasalimu amri.

NATO Generalsekretär Anders Fogh Rasmussen NATO Treffen
Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh RasmussenPicha: AP

Anders Fogh Rasmussein ni katibu mkuu wa Jumuiya hiyo alisema " NATO inawataka Walibya waamue juu ya hatima yao kwa njia ya amani na ya uhuru, leo wanaweza kujenga hatima hiyo"

Akizungumza na Shirika la Habari la Ufaransa AFP, mwanadiplomasia mmoja ambae hakutaka kutajwa jina alisema alikutana na Gaddafi katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Makaazi ya Bab al-Aziziya yameshambuliwa mara kadhaa na makombora ya NATO, tangu kuanza kwa operesheni ya kuzuia ndege kuruka kwa lengo la kuwalinda raia wa Libya Machi 19,Sehemu kubwa ya majengo yameharibiwa.

Hata hivyo chanzo hicho kilisema Gaddafi ana maandaki mengi.

Waasia ambao wanadaiwa kuudhibiti mii wa Tripoli kwa zaidi ya asilimia 80 wakiwa na magari yaliyosheheni silaha nzito nzito hivi sasa wanamiminikia uwanja wa Kijani mjini Tripoli.

Makundi kwa makundi yakisikika yakiswema Allahu Akbar, ikimaanisha mungu mkubwa na kuongeza kwamba Gaddafi amemalizika.

Mwandishi: Sudi Mnette/ AFP
Mhariri:Abdul-Rahman