1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Libya wadai kuukaribia ushindi

18 Agosti 2011

Waasi wa Libya leo wameendelea kujaribu kuingia mji wa Tripoli na huku wakidai kwamba wamedhibiti kituo kituo muhimu cha kusafishia mafuta, wakati kiongozi wao akionesha shaka ya kutokea mapigano makali zaidi.

https://p.dw.com/p/12J4g
Waasi wakishangiliaPicha: dapd

Kutokana na matarajio ya ushindi, viongozi waasi kwa hivi sasa wapo katika mchakato kuliondoa taifa hilo kutoka katika udikteta na kuelekekeza katika demokrasia kamili. Mpango mkakati huo unatarajiwa kuliongoza taifa hilo katika miongo kadhaa ijayo.

Akizungumza na gazeti mmoja mjini Benghazi, Kiongozi wa Baraza la Mpito la Waasi, Mustafa Abdel Jalil amesema kuna shaka ya kutokea mapigano yatakayosababisha umwagikaji damu mkubwa mjini Tripoli kututokana na Gaddafi kukaidi kujiuzulu.

Libyen Mustafa Abdel Jalil 13. August 2011
Mwenyekiti wa TNC Mustafa Abdel JalilPicha: picture alliance/dpa

Jalil alisema" Gaddafi hawezi kuondoka kimyakimya, ataondoka kwa kusababisha janga kubwa litakalomgusa yeye binafsi na familia yake" kiongozi huyo aliliambia gazeti liinaloitwa "Asharq Al-Awsat".

Gaddafi amekuwa akiongoza nchi hiyo ya Afrika ya Kaskazini yenye utajiri mkubwa wa mafuta kwa miongo minne na amekuwa akikaidi kujiuzulu na kufanya mashambulizi dhidi ya waandamanaji.

Jalil anasema ana matumani kwamba atasheherekea sikuku ya Eid al-Fitr mjini Tripoli, baada ya mfungo wa ramadhani ambao unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Waasi alirejea kauli yake inayoeleza" hakuna suluhu yeyote itakayofikiwa kama haitahusisha kuondoka kwa Gaddafi na mwanawe nchini humo"

Jalili alikuwa akimkosa mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Abdel Ilah Khatib, ambae aliwasilisha mapendekezo yake nchini humo ambayo hayakugusia matakwa hayo.

Kiongozi huyo wa waasi alikanusha madai ya kufanyima mazunguzo kati yao na utawala wa Gaddafi huko nchini jirani ya Tunisia.

Mapambano yanaendelea, waasi wapo katika jitihada ya kulikata bomba la mafuta ambalo linapeleka malighafi hiyo katika mji wa Tripoli, mji wa uzawa wa Gaddafi, Sirte huko mashariki mwa nchi hiyo.

Shabaha ya jitihada hiyo ni kuufanya mji wa Tripoli usikalikea, hali ambayo imekwishaanza kujidhihirisha. Hivi sasa kumekuwa na tatizo la umeme na mtandao wa mawasilianao ya simu umekuwa duni.

Huko katika mji wa Zawiyah, waasi wanadai kudhibiti sehemu kubwa ya mji huo wenye hazina ya mafuta kasoro upande wa mashariki.

Mwandishi: Sudi Mnette/AFP
Mhariri:Abdul-Rahman,Mohammed