1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAPUTO:Watu 83 wapoteza maisha kwenye mlipuko wa ghala la silaha

23 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGA

Yapata watu 83 wamepoteza maisha yao kufuatai moto uliosababishwa na mlipuko kwenye ghala la silaha la kitaifa mjini Maputo nchini Msumbiji.Kwa mujibu wa Waziri wa Afya Ivo Garrido takriban watu 300 wamejeruhiwa na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka.Majeruhi hao walijumuisha wafanyikazi wa jeshi vilevile raia wa kawaida wanaoishi kwenye maeneo ya karibu.

Chanzo cha mlipuko huo wa jana mchana hakijajulikana.Rais Armando Guebuza wa Msumbiji alikatiza ziara yake ya siku moja nchini Afrika Kusini anatoa wito kwa utulivu kudumishwa.Kadhalika ameahidi kuhamishwa kwa ghala hilo kwenye eneo hilo hadi nje ya mji. Majengo kadhaa katikati ya mji yalitikisika na madirisha kuvunjika pale mlipuko huo ulipotokea.Ghala hilo la silaha linatumika kuhifadhi bunduki na risasi nyinginezo zilitumika wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kulingana na msimamizi wa Shirika la Msaada la Msalaba Mwekundu, Redcross Bi Unice Mucaphe mitaa minane imeathiriwa na watu bado wanaendelea kuhamishwa.

Serikali ya Msumbiji iko katika harakati za kuharibu silaha za zamani zilizohifadhiwa katika ghala hilo.