1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya kombe la Shirikisho la kandanda la Ujerumani.

16 Agosti 2010

Bayern Munich Kupambana na Schalke 04.

https://p.dw.com/p/Ooru
Christoph Metzelder wa Schalke,kulia,na Thomas Mueller wa Bayern Munich waking'ang'ania mpira katika mpambano uliopita.Picha: AP

Katika michuano ya kombe la Shirikisho la kandanda la Ujerumani DFB, miongoni mwa  matukio ya kushangaza ni kuyaaga mashindano mapema kwa kilabu ya St Pauli iliopanda daraja  kucheza ligi kuu bundesliga msimu huu. St Pauli ilitandikwa  bao moja kwa bila na  kilabu ya daraja la nne Chemnitz .

Kilabu nyengine ya  ligi kuu iliyopata pigo na kuyaaga mashindano haya mapema ni Hannover baada ya kutolewa na  kilabu inayocheza ligi ya mkoa ya Eversberg  kwa mikwaju ya Penalty mabao 5-4 baada ya kumaliza dakika za kawaida  za nyongeza zikiwa bado sare bila kwa bila .

 Lakini mvua ya magoli iliwakumba wachezaji wa ridhaa kutoka Torgelower mbele ya  Hamburg iliyowamiminia  mabao 5-1 . Mdachi Ruud van Nisrelrooy aliuona wavu mara tatu.

 Bremen haikua na kazi ngumu na hivyo ikaiondoa timu ya daraja la tatu Rot Weisse  4-0, huku Wolfsburg na kocha wao Muingereza Steve McClaren ikilazimika kutoka jasho jembamba hadi dakika mbili kabla ya mchezo kumalizika ndipo ilipopata ufuweni kwa bao la ushindi la Mbrazil Grafite na pambano lao kumalizika kwa magoli 2 kwa 1.

Leo katika mashindano ya kombe hilo la shirikisho la kandanda  la Ujerumani Bayern Munich, mabingwa wa Ujerumani wataumana na  Schalke.

Akizungumzia mpambano huo mchezaji wa Bayern Munich Thomas Müller alikuwa na haya ya kusema.

Itakumbukwa kuwa Müller aliibuka mojawapo ya wachezaji bora katika mashindano yaliomalizika ya kombe la dunia nchini Afrika kusini.

Mwandishi Maryam Dodo Abdalla

Mpitiaji:Abdul-Rahman, Mohammed