1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Baraza la mawaziri kupangwa upya Urusi

13 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQ3

Waziri Mkuu mteuliwa wa Urusi,Viktor Subkov alipozungumza bungeni hii leo,alisema anatazamia kulipanga upya baraza la mawaziri.Subkov vile vile amesema,huenda akagombea uchaguzi wa rais utakaofanywa mapema mwakani.Subkov amependekezwa na Rais Vladimir Putin kuchukua nafasi ya Michail Fradkov aliejiuzulu kama waziri mkuu siku ya Jumatano baada ya kushika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu.

Bunge linatazamiwa kumuidhinisha Subkov litakapokutana siku ya Ijumaa.Fradkov amesema, amepaswa kujiuzulu ili kutoa nafasi kwa baraza la mawaziri kufanya matayarisho ya chaguzi za bunge katika mwezi wa Desemba na uchaguzi wa rais utakaofanywa mwezi Machi mwaka 2008.