1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Watu sita wajeruhiwa katika shambulio la bomu

19 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQu

Watu wasiopungua sita wamejeruhiwa kufuatia mlipuko uliosababishwa na bomu kwenye mkahawa wa McDonalds mjini St Petersburg nchini Urusi. Waathiriwa wa shambulio hilo wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya mjini humo.

Maofisa wamesema mlipuko huo umesababisha uharibufi mkubwa kwa mkahawa huo. Msemaji wa polisi mjini St Petersburg amethibitisha kuwa mripuko huo ulisababishwa bomu ambalo inaaminiwa lilikuwa limetegwa chiniy a meza.

Kufikia sasa haijabainika ikiwa mlipuko huo umefanywa na gaidi au ni kitendo cha uhalifu.