1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSUL:Idadi ya waliokufa kwenye shambulio la Nineveh yaongezeka

15 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYq

Zaidi ya watu 200 wamepoteza maisha yao pale shambulio la bomu lilipotokea kwenye eneo la Nineveh kaskazini mwa Iraq na kulenga madhehebu ya Yazidi.Shambulio hilo lilitokea baada ya malori manne yaliyosheheni mabomu kulipuka.Hilo ni shambulio baya zaidi kutokea na kusababisha vifo vingi kwa mpigo mmoja nchni Iraq tangu uvamizi kutokea.Maiti nyingi zinaaminika kunasa kwenye vifusi.

Wazir Mkuu wa Iraq Nuri al maliki aliwalaumu wapiganaji walio na msimamo mkali kwa kutekeleza kitendo hicho cha kihalifu.Mashambulio ya vijiji vya Al-Qathaniya na Al-Adnaniyah yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 200 na wengine 200 kujeruhiwa.Hayo ni kwa mujibu wa meya wa baraza la Sinjar Dakhil Qassim Hassun.

Kulingana na maafisa wa serikali wahanga walipekwa kwenye hospitali za eneo hilo la kaskazini huku juhudi za uokozi zikiendelea.Yapata nyumba 70 ziliporomoshwa na shambulio hilo jambo lililowafanya polisi kutangaza muda wa kutotembea kwenye eneo la Sinjar vilevile mji ulio karibu wa Tal Afar.

Marekani kwa upande wake inakashifu shambulio hilo lililoathiri maisha ya raia wasio na hatia na kuahidi kusaidia majeshi ya usalama ya Iraq kupambana na wauaji hao.

Wakati huohuo Iraq inajiandaa kuunda kundi la wataalam watakaoshughulikia masuala ya ugaidi na kuimarisha usalama katika eneo la mpaka na nchi ya Jordan.Kwa mujibu wa mshauri wa usalama wa kitaifa wa Iraq Muwaffaq al Rubaie kundi la wataalam watakaoshirikiana katika masuala ya usalama na ujasusi linapangwa kuundwa.Kiongozi huyo aliyasema hayo baada ya kumaliza mkutano wa siku mbili na maafisa wa ngazi za juu wa Jordan uliofanyika mjini Amman.

Kulingana na Bwana Rubaie Iraq inakabiliwa na matatizo ya kiusalama yanayozonga ufalme wa Jordan.Jordan imeimarisha mpaka wake na Iraq kufuatia shambulio la mwaka 2005