1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muscat: Hamna hata mwanamke mmoja aliyeshinda katika uchaguzi wa baraza la ushauri la Oman

28 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Bw

Hamna hata mwanamke mmoja aliyechaguliwa kati ya wanawake 21 waliopigania katika uchaguzi wa baraza la ushauri lenye wanachama 84 huko Oman. Baraza hilo halina usemi mkubwa katika mambo ya serekali ya nchi hiyo. Mwaka 2003 wanawake wawili walishinda kuingia katika baraza hilo katika nchi hiyo inayotawaliwa na Mfalme Qaboos.